
Serikali imesema hakutakuwa na uhamisho wa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwenye shule za kutwa kuhamia bweni kwani upangaji wa shule kwa wanafunzi hao umefuata vigezo na taratibu.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu, Wizara ya TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe, ambapo amebainisha kuwa tangu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe.Angellah Kairuki atoe taarifa ya kuwapangia shule wanafunzi wa kidato Cha kwanza mwaka 2023, ofisi hiyo imepokea maombi mengi toka kwa wazazi kuomba watoto wao kuhamia shule za bweni kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za ugonjwa au matamanio ya wazazi.
Kutokana na hali hiyo, Profesa Shemdoe amesema hakuna uhamisho wa wanafunzi waliochaguliwa kutwa kwenda bweni kwani upangaji wa umefuata vigezo na taratibu.
" Na kwa wanafunzi wenye changamoto za kimazingira, mfano amehama makazi ya awali wawasilishe changamoto hizo kwa Makatibu Tawala wa Mkoa ili zitatuliwe, maana upangaji wa wanafunzi kwenye shule umezingatia ukaribu wa shule na makazi ya wanafunzi hivyo endapo wamehama makazi ya awali kunaweza kutokea changamoto ya umbali.
Profesa Shemdoe amesema kupangiwa shule kwa wanafunzi kumezingatia viwango vya ufaulu, ushindani pamoja ukaribu wa shule na makazi.
Aidha, idadi ya wanafunzi waliopangiwa kwenye shule za bweni imezingatia viwango vya juu vya ufaulu na nafasi zilizokuwepo ktk shule hizo ili kuepusha msongamano kwa wanafunzi darasani na mahali pakulala.
Endapo zitatokea nafasi za bweni zitakazohitajika kujazwa hapo baadae, maombi yatakayokuwa yamefikishwa Ofisi ya Rais-TAMISEMI yatachambuliwa na kamati maalum ambayo itaangalia sifa za walioomba kuhamishiwa huko.
Aidha, Prof. Shemdoe ametoa wito kwa wazazi kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa wanaripoti shuleni kwa wakati na kwamba hakutakua na chaguo la pili la mwanafunzi.
" Kwa mwaka huu hakutakuwa na chaguo la pili la wanafunzi kwasababu fedha zilizotolewa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan katika sekta ya elimu zimetosha kuboresha
