Back to top

HALI BADO MBAYA GAZA, MASHAMBULIZI 3 YAUA TENA.

17 July 2024
Share

Takriban watu 48 wameuawa katika mashambulizi matatu ya anga ya Israel ndani ya saa moja siku ya Jumanne, kwa mujibu wa shirika la ulinzi wa raia wa Gaza.

Mashambulizi hayo yameua takriban watu 25 katika shule inayosimamiwa na Umoja wa Mataifa, katika eneo la Nuseirat katikati mwa Gaza, 18 waliuawa Kusini mwa Khan Younis, na watu watano waliuawa huko Beit Lahiya Kaskazini mwa Gaza.

Umoja wa Mataifa umesema shambulizi la Israel lilipiga karibu na kituo chake cha operesheni ya pamoja huko Deir el-Balah, ambapo inaratibu taratibu za misaada ya kibinadamu huko Gaza.

Katika miezi tisa ya vita, asilimia 70 ya shule za zinazosimamiwa na umoja wa mataifa (UNRWA) huko Gaza sasa zimeshambuliwa kwa mabomu na watu 539 waliokuwa wamejihifadhi ndani ya majengo yake wameuawa.

Takriban watu 38,713 wameuawa na 89,166 wamejeruhiwa katika vita vya Israel dhidi ya Gaza tangu Oktoba 7.

 Idadi ya vifo nchini Israel kutokana na mashambulizi yaliyoongozwa na Hamas Oktoba 7 inakadiriwa kuwa 1,139, na makumi ya watu bado wanazuiliwa mateka huko Gaza.