Back to top

Hali ya chakula nchini ni nzuri .    

20 July 2019
Share

Waziri wa kilimo na chakula Mh Josephat Hasunga amesema hali ya chakula nchini ni nzuri kutokana na uzalishaji wa mazao ya ziada na  chakula kuwepo kwa wingi kwa mwaka 2019/2020.

Mh Hasunga ameyasema hayo alipokuwa akitoa tathimini ya hali ya chakula alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

Aidha waziri huyo mwenye dhamana ya kilimo na chakula nchini amewaagiza wataalamu wa kilimo na mamlaka ya mapato waliopo mpakani wanahakiksha kuna kuwepo na usimamizi wa kina kujua na kupata takwimu za kina ya vyaakula vinavyotoka nje ya nchi.