Back to top

Halimashauri zatakiwa kutenga fedha kwa ajili ya matumizi ya Ardhi.

20 April 2018
Share

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.Wiliam Lukuvi amezitaka halimashauri zote nchini kuhakikisha zinatenga fedha kwa ajili ya kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa ajili ya upimaji wa Ardhi.

Amesema wizara yake imekwisha kuweka mipango mikakati ya kuhakikisha  ardhi yote ya Tanzania inapangwa, inapimwa, na kumilikishwa kisheria, ambapo miongoni mwa mikakati hiyo ni kupima, na kumilikisha kila kipande cha ardhi hapa nchini.

Waziri Lukuvi ameliambi Bunge kuwa ni azma ya wizara yake inafanya kila liwezekanalo inapima ardhi yote nchini kama moja ya kupunguza migogoro ya ardhi hasa kati ya wakulima na wafugaji.

Akijibu swali la Mbunge wa Karatu Mh. Qambalo Will aliyetaka kujua mkakati wa serikali wa kuipima ardhi yote nchini Mh.Lukuvi amesema wizara yake imekuwa ikizijengea uwezo mamlaka za upangaji katika kuandaa mipango ya ardhi.