
Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba amesema gharama ya vifaa vya kuunganisha umeme ni kubwa sana na hakuna mtanzania anachajiwa gharama ya huduma (Service Charge) pale anapohitaji kuunganishiwa umeme ambayo ukipiga hesabu ni zaidi ya Tshs. 600,000/=.
.
Mhe. Makamba amesema hayo akiwa ziarani katika kijiji cha Kilando kilichopo wilayani Nkasi, mkoani Rukwa baada ya wananchi hao kuwasilisha kero ya gharama kubwa za kuunganishiwa umeme ambapo Waziri Makamba akabainisha kuwa, kwa mtanzania wa mjini analipa 320,000 na wa kijijini 27,000 tu.
