
Wabunge nchini Somalia wamemchagua Bw.Hassan Sheikh Mohamud kuwa Rais wa nchi hiyo kwa kura 214 akimshinda Rais aliyepo madarakani Mohammed Abdullahi Farmajo aliyepata kura 110 ambaye amekuwa akihudumu katika nafasi hiyo tangu mwaka 2017.
Uchaguzi huu ambao ulikuwa na ushindani mkali ulitarajiwa kufanyika mwaka uliopita wakati muhula wa miaka minne wa Bw.Farmajo ulipokamilika lakini tofauti za kisiasa na usalama zikichelewesha uchaguzi huo huku Rais aliyekuwa akihudumu akisalia madarakani.
Bw.Hassan Sheikh Mohamud aliapishwa muda mfupi baada ya matokeo ya mwisho kutangazwa akirudi katika nafasi anayotarajia kuishikilia tena kwa miaka minne ijayo kwakua alishawahi kuishikilia kati ya mwaka 2012 hadi 2017.
Rais Hassan Mohamud atalazimika kukabiliana pamoja na mambo mengine athari za ukame ambao umoja wa mataifa unasema takriban raia milioni 3.5 wako hatarini kukumbwa na kiangazi cha kiwango cha juu na kukomboa eneo kubwa la taifa hilo ambalo lipo chini ya udhibiti wa kundi la wapiganaji wa Alshabab.
