Back to top

Hatua za kudhibiti homa ya manjano nchini.

09 March 2022
Share

Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu amewataka wananchi kuchukua tahadhari, na kujua dalili za ugonjwa wa homa ya manjano kama homa, kuumwa kichwa, maumivu ya misuli na mgongo, mwili kutetemeka, kupoteza hamu ya kula, kichefuchefu na kutapika, mwili kuwa na manjano, kutokwa na damu sehemu za wazi.

Waziri Ummy ameyasema hayo wakati akitoa tahadhari ya kuzuka kwa ugonjwa wa Homa ya Manjano (Yellow Fever) ambapo amesema tarehe 03 Machi 2022 Wizara ya Afya ilipokea taarifa kutoka WHO hapa nchini ikielezea kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa homa ya manjano nchini Kenya.

Pia Waziri Ummy ameagiza Hospitali zote za rufaa nchini kuwa na huduma za kupima na kutoa chanjo ya homa ya manjano kwa wasafiri na wenye uhitaji na pia ameagiza maafisa wa afya mipakani kuhakikisha wasafiri wanaoingia kutoka nchi zenye maambukizi wanakua na vyeti vya chanjo.