Back to top

HELiKOPTA YA JESHI YAANGUKA KENYA, WATANO WAFARIKI

18 April 2024
Share

Watu watano wamefariki dunia huku watatu wakijeruhiwa ,baada ya helikopta ya Jeshi la Kenya (KDF), kuanguka na kuwaka moto, katika eneo la Cheptulel , lililopo Kaunti ya West Pokot, wakati ikiruka.
.
Imeelezwa kuwa, helkopta hiyo ilikua imebeba Maafisa wa ngazi za juu wa Jeshi hilo, akiwemo Mkuu wa Majeshi ya Vikosi vya ulinzi vya Kenya, Meja Jenerali Francis Ogolla, na walikuwa wakitembelea Kaunti za North Rift zinazokabiliwa na mashambulizi ya wavamizi.