Back to top

HERSI AWEKA HISTORIA, AWA M/KITI WA KWANZA WA ACA

30 November 2023
Share

Rais wa Klabu ya soka ya Yanga, Injinia Hersi Said (@caamil_88), amechaguliwa kuwa  Mwenyekiti wa kwanza wa Shirikisho la Vilabu Afrika - African Clubs Association (ACA).
.
Hersi amechaguliwa kushika nafasi hiyo katika kikao cha uzinduzi wa Shirikisho hilo kilichofanyika Jijini Cairo nchini Misri, ambapo nafasi hiyo inamuingiza moja kwa moja, Rais huyo wa Yanga kwenye Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF Executive Commitee).