
Watu wa 6 wamefariki dunia na wengine 19 wamejeruhiwa, baada ya basi dogo la abiria, aina ya Hiace, lenye namba za usajili T339 DBV lililokuwa likitokea Kata ya Izimbya Wilaya ya Bukoba kwenda Manispaa ya Bukoba, kufeli breki na kugonga watu, pikipiki na nguzo za umeme kisha kuaguka katika eneo la mteremko wa Katerero.
Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera, Kamishina Msaidizi wa jeshi hilo , Bw.Blasius Chatanda, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema majeruhi na waliofariki dunia wamepele kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mjini Bukoba.
Katika hatua nyingine Kamanda huyo wa Mkoa wa Kagera, Blasius Chatanda, amekitaja chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi hilo kushindwa kufunga breki baada ya gari hilo kufeli breki.
