Back to top

HOMA YA LASSA YAUA 37 NIGERIA

04 February 2023
Share

Watu 37 wamefariki dunia nchini Nigeria kwa homa ya Lassa ambayo virusi vyake vinasambazwa na panya wa kawaida. Kituo cha Kudhibiti Magonjwa cha nchi hiyo kimesema kimezindua kituo cha dharura cha kuratibu, na kuimarisha shughuli za kuudhibiti.

Mkurugenzi Mkuu wa kituo hicho Bwana Chikwe Ihekweazu, amesema hali ya hatari imetangazwa baada ya tathmini kubaini kuwa homa hiyo inasambaa kwa kasi kubwa.

Amesema mwaka huu kumeshuhudiwa kuongezeka kwa idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa, ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Kituo hicho kimesema hadi juzi kulikuwa na watu mia mbili arobaini na wanne waliothibitishwa kuugua na thelathini na saba miongoni  mwao wamefariki dunia kwa ugonjwa huo.