Back to top

HOSPITALI KONGWE NCHINI ZATENGEWA BILIONI 21

11 April 2022
Share


Serikali imesema katika mwaka wa fedha 2022/23 imetenga shilingi bilioni 21 kwa ajili ya ukarabati wa hospitali kongwe 21 ambapo kupitia mpango huo kila hospitali kongwe itapewa shilingi bilioni 1 kwa ajili ya ukarabati.

Kauli ya serikali imetolewa bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe.Festo Dugange wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum Mhe. Mwantumu Mzamiru Zodo ambaye aliuliza je ni lini serikali itafanya ukarabati wa hospitali ya Wilaya ya Pangani.

Aidha Mhe.Dugange akijibu swali hilo ameongeza kwamba serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kukarabati hospitali za halmashauri ambazo miundombinu yake imechakaa ili kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini huku akimhakikishia mbunge wa viti maalum Mhe.Mwantumu Zodo miongoni mwa hospitali ambazo zitafanyiwa ujenzi na ukarabati ni hospitali ya Wilaya ya Pangani.