Back to top

hospitali ya Benjamin Mkapa kupandikiza figo ni hatua kubwa.

27 March 2018
Share

Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan amesema hatua ya hospitali ya Benjamin Mkapa kuweza kufanya upandikizaji wa figo ni hatua kubwa kwa maendeleo ya taifa katika sekta ya afya.

Amesema hayo mkoani Dodoma na kuongeza kuwa serikali inajivunia hatua hiyo na kwamba inafuatilia kwa karibu afya ya mgonjwa aliyepandikizwa figo wiki iliyopita.

Amesema gharama za upandikizaji figo katika hospitali hiyo ambazo ni chini ya shilingi milioni ishirini na mbili zinaweza kukusanywa katika ngazi za familia na kuokoa maisha ya mgonjwa.

Wiki iliyopita madaktari wa hospitali ya Benjamin Mkapa kwa kushirikiana na wale wa kutoka nchini japan walifanikiwa kufanya upandikizaji wa kwanza wa figo kwa mgonjwa katika hospitali hiyo.

Upandikizaji huo unafanya mpaka sasa Tanzania kuwa na hospitali mbili zenye uwezo wa kupandikiza figo ambayo ni hospitali ya Muhimbili na hiyo ya Benjamin Mkapa.