Mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Pololeti Mgema amewataka wasimamizi wa hospitali,zahanati na vituo vya afya zinazomilikiwa na na madhehebu ya dini wilayani humo kuhakikikisha wanatoa huduma kwa gharama nafuu kulingana na msamaha wa kodi wanaoupata wanapoagiza vifaa na madawa kutoka nje ya nchi.
Bw. Mgema ameyasema hayo wakati akizindua mashine ya kisasa ya kuchomea taka ya hospitali ya Rufaa ya misheni peramiho iliyonunuliwa toka Korea Kusini kwa zaidi ya shilingi Milioni 200 ambapo katika wilaya ya Songea Kanisa Katoliki linamiliki vituo vya afya,zahanati na hospitali nyingi mijini na vijijini likisaidiana na serikali katika kutoa huduma za afya.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa hospitali ya Rufaa ya misheni Peramiho Dk Ansigar Stuffe amesema wamenunuma mashine hiyo ili kutunza mazingira na kuondoa athari za taka kwa wagonjwa na wanakuja kuuguza wagonjwa kwa kuwa mashine hiyo haitoi moshi wakati wa kuchoma taka.