Back to top

HOSPITALI ZA SERIKALI NA BINAFSI ZISHIRIKIANE

07 January 2023
Share

Naibu Waziri wa Afya, Mhe. Godwin Mollel ameelekeza wataalamu wa afya katika hospitali za serikali na binafsi nchini, kuendelea kuimarisha ushirikiano katika utendaji ili kuongeza tija na ufanisi katika kuwahudumia wananchi.
.
Dkt.Mollel ametoa maelekezo hayo alipofanya ziara ya kuangalia hali ya utoaji huduma katika hospitali Ruthelani iliyokuwa ikifanya kazi kama hospitali ya Wilaya na hospitali ya Wilaya ya Karatu iliyokamilika na kuanza kutoa huduma hivi karibuni.
.
Aidha, Dkt. Mollel amemwelekeza Meneja wa MSD kanda ya Kaskazini kuhakikisha ndani ya mwezi huu, Januari analeta vifaa na vifaa tiba na dawa ambavyo fedha yake ipo kwenye akaunti ya MSD ili wananchi wengi zaidi waanze kunufaika na uwekezaji huo mkubwa uliofanywa na Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan.