Back to top

Hospitali zapigwa marufuku kuzuia maiti.

09 June 2021
Share

Siku moja baada ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kupiga marufuku hospitali kuzuia maiti, Katibu Mkuu Wizara Afya, Maendeleo Ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Prof. Abel Makubi amepiga marufuku watendaji wa hospitali na vituo vya afya vyote vilivyopo nchini kuzuia maiti inayotakiwa kuchukuliwa na ndugu.
.
Katika agizo hilo ambalo amelitoa Jijini Dodoma Prof.Makubi amesema tayari miongozo na barua  mbalimbali kuhusu suala hilo imeshasambazwa katika vituo vya afya na hospitali zote nchini.