Back to top

Hussein Mwinyi kuboresha miundombinu ya Elimu Zanzibar.

15 October 2020
Share

Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt.Husein Ali Mwinyi amesema endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar ataboresha miundombinu ya elimu.

Katika uboreshaji huo Dkt.Mwinyi amesema atajiri walimu wapya wa sayansi na hisabati ili kuongeza ufaulu sambamba na kuipandisha daraja hospitali ya Micheweni kuwa ya wilaya.

Dkt.Mwinyi amesema hayo kwenye mkutano wa kampeni uliohudhuriwa na viongozi mbali mbali wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo Rais Dkt.Ali Mohamed Shein.

Mgombea huyo amesema akiwa Rais wa ameahidi kujenga bandari ya Nshumba kujenga soko la samaki ili kuongeza kasi ya ufanisi katika bandari hiyo.

Mapema Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein amewataka wananchi wa Micheweni kumchagua Dkt.Mwinyi kwa vile anasifa zote zakuwa rais wa Zanzibar.

Rais wa Zanzibar  - Dkt.Ali Mohamed Shein