Back to top

Idadi kubwa ya viwanda vidogo nchini vimedorora kwa kukosa mitaji.

10 October 2018
Share

Idadi kubwa ya  viwanda vidogo vya kuchakata vyakula matunda ngozi na mafuta ya kula  hapa nchini vimedorora kutokana na kukosa mitaji kunakodaiwa kusababishwa na ukosefu wa mipango mizuri ya uendeshaji biashara.

Mkurugenzi Mkuu wa  Shirika la kuendeleza viwanda vidogo  SIDO Prof Silvester Mpanduji ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wadau wa viwanda vidogo pamoja na watalam wa biashara  na mikopo kutoka SIDO  wanaokutana jiji  Arusha.


Meneja wa Mikopo kutoka SIDO Makao Makuu Haika Shayo anasema kinachoangusha wafanyabiashara wadogo ni kukosa utaalam wa kuandaa maandiko yatakayokubalika kwenye taasisi za fedha.