Back to top

IDADI YA VIFO JOHANNESBURG YAFIKIA 74

31 August 2023
Share

Takriban watu 74 wakiwemo watoto 12, wamefariki na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa, baada ya moto kuteketeza jengo la ghorofa tano katikati mwa Johannesburg nchini Afrika Kusini, ambalo lilikuwa limegeuzwa kuwa makazi yasiyo rasmi.

Mamlaka imesema wamepita kwenye ghorofa moja hadi ghorofa nyingine, wakitafuta manusura na kutoa miili.Huku wakisema kuna uwezekano idadi ya vifo ikaongezeka.

Maafisa wa Uokoaji wamesema moto huo sasa umezimwa.