Back to top

Idadi ya wagonjwa wa COVID-19 nchini Kenya yaongezeka

20 June 2020
Share

Idadi ya maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 nchini Kenya imeongezeka na kufikia watu 4,478 baada ya wagonjwa 104 kuthibitishwa katika muda wa saa 24 zilizopita huku wote wakiwa raia wa Kenya.

Wizara ya afya inasema kuwa sampuli 2,820 zinachunguzwa katika maabara mbalimbali nchini.

Naibu waziri wa afya Dkt.Rashid Aman anasema kuwa miongoni mwa waliothibitishwa kuambukizwa ni mtoto wa mwaka mmoja.
Maambukizi ya hii leo yakiwa ni pamoja na 60 kutoka jijini Nairobi na 33 kaunti ya Mombasa.

Wakati huo huo idadi ya waliopona imeongezeka na kufikia watu 1,586 baada ya watu 36 zaidi kupona na kuruhusiwa kuondoka hospitalini.

Hata hivyo waliofariki wamefikia 121 baada ya watu 2 zaidi kuaga dunia.