Back to top

Idara ya uhamiaji mkoa wa Singida inawashikilia wahamiaji haramu 22.

07 February 2019
Share

Idara ya uhamiaji mkoani  Singida ina washikilia wahamiaji haramu ishirini  na mbili wakiwemo familia tatu zenye watoto kutoka  nchi za Burudi ,Kenya na Somalia ,ambao walikuwa wakisafiri kwa basi  kutoka Tabora kupitia mkoani Mbeya hadi nchi ya Malawi kwa ajili ya kutafuta maisha .    

Afisa uhamiaji mkoa wa Singida  Kamishina msaidizi Bi .Anjela Shija amethibitisha kukamatwa kwa raia hao katika kijiji cha Rungwa tarafa ya Itigi wilayani Manyoni  na kusema kuwa walikuwa wakisafirishwa na basi la Sasebosa lenye usajili wa namba T 288 BBM.