Back to top

IGP Simon Sirro awaonya wanaojipanga kufanya funjo uchaguzi mkuu.

03 July 2020
Share

ARUSHA.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewaonya watu wanaotegemea kufanya fujo kipindi cha uchaguzi mkuu na kusema watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza na maofisa wa Jeshi hilo jijini Arusha IGP Simon Sirro amewahakikishia wananchi kuwa uchaguzi utakwenda vizuri kama ulivyopangwa na jeshi hilo litaendelea kutenda haki.

Amesema askari wa Jeshi hilo wamepata mafunzo ya kutosha yatakayowawezesha kukabiliana na matishio mbalimbali ikiwemo uhalifu na wahalifu pamoja na mbinu nyingine za kuwashughulika wanaovunja sheria na kuwataka askari wa jeshi hilo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi.