Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro amewatembelea majeruhi wa ajali iliyotokea wilayani Mufindi wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa na kuwapa pole kufuatia ajali waliyoipata.
IGP Sirro pia amefika na kukagua eneo ilipotokea ajali iliyosababisha vifo pamoja na majeruhi kadhaa, ambao wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa.
