Back to top

IGP WAMBURA AAGIZWA KUSIMAMIA SHERIA

02 December 2022
Share

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Jumanne Sagini, amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Camillus Wambura, kuhakikisha anasimamia kikamilifu sheria za usalama barabarani, hususani katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa mwaka.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha 16 cha Baraza la wafanyakazi wa Idara ya Jeshi la Polisi kilichofanyika Jijini Dodoma Mhe. Sagini amesema kuwa, ni vyema wananchi wakaendelea kushirikiana na serikali kupaza sauti kukemea ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikisababisha vifo na majeruhi.

Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura amesema kuwa, ili kufikia malengo ya serikali ya kuwa na Jeshi la Polisi lenye kutenda kwa nidhamu, haki, weledi na uadilifu, Jeshi limeendelea kulinda usalama wa raia na mali zao pamoja na kukabiliana na matukio na matishio mbalimbali ikiwemo uwepo wa makosa ya mmomonyoko wa maadili kwenye jamii.