Back to top

IHEFU SC SASA NI SINGIDA BLACK STARS SC

02 April 2024
Share

Timu ya Soka ya Ihefu SC, inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara, imetangaza kubadilisha jina la timu hiyo kutoka IHEFU SPORTS CLUB  na sasa itaitwa SINGIDA BLACK STARS SPORTS CLUB.
.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Uongozi wa timu hiyo, umesema malengo ya kubadili jina hilo ni kuiunganisha timu na wananchi wote wa Mkoa wa Singida na kwamba taratibu zote za usajili wa jina hilo zimekamilika.
.
Maamuzi hayo yanafuata ikiwa miezi michache tu, tangu timu hiyo ihamishe makazi yake kutoka Mbarali mkoani Mbeya na kwenda mkoani Singida.