Back to top

"ISRAEL HAINA BUDI KUONDOA VIZINGITI"-GUTERRES

25 March 2024
Share

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema Israel haina budi kuondoa vizingiti vilivyosalia pamoja na vituo vya ukaguzi ili kufanikisha ufikishwaji wa misaada Gaza.

Guterres ametaka Israel kuweka mazingira rahisi ili kuhakikisha misaada muhimu inaingizwa kwenye Ukanda wa Gaza unaokabiliwa na kitisho cha njaa.

Guterres amesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Cairo sambamba na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Sameh Shoukry na kutoa wito kwa mara nyingine wa usitishwaji wa mapigano ili kupunguza madhila yanayowakabili Wapalestina, wanaopambana kwenye mazingira magumu yaliyoko Gaza.

Guterres hapo jana alitembelea kivuko cha mpakani cha Rafah kinachopakana na Gaza katikati ya miito inayoongezeka dhidi ya Israel ya kupunguza vizuizi na kufungua vivuko ili kuruhusu misaada kuingia Ukanda wa Gaza.