Back to top

ISRAEL KUANZA OPERESHENI ZA ARDHINI.

06 December 2023
Share

Mapigano makali yameendelea kuripotiwa katika Ukanda wa Gaza ambako Jeshi la Israel limetangaza kuwa kwa mara ya kwanza limeanzisha operesheni kubwa ya ardhini na wamefanikiwa kukizingira kabisa kitongoji cha Khan Younis.

Wakati wito wa kuwalinda raia ukiendelea kutolewa, Jeshi la Israel limeapa kuliangamiza kundi hilo la Hamas na pia limewataka wakazi kuhama kutoka sehemu za Kusini mwa Gaza na kuelekea katika maeneo salama yaliyotengwa ili kuepuka mapigano hayo.

Mkuu wa shirika la Marekani la Maendeleo na Misaada ya Kimataifa (USAID) Samantha Power amesema msaada mpya wa Marekani wa dola milioni 21 utatolewa kwa ajili ya watu wa Gaza, na msaada huo utaelekezwa katika sekta za usafi, makazi na chakula.