Back to top

ISRAEL YAWAUA KIMAKOSA RAIA WAKE WATATU

16 December 2023
Share

Jeshi la Israel (IDF) limewaua kimakosa raia wake watatu, waliokuwa wametekwa na Hamas, ambapo limebainisha kuwa raia hao walipigwa risasi na wanajeshi wanaoendesha harakati za kijeshi katika eneo la Shejaiya, kaskazini mwa Gaza.
.
Kufuatia tukio hilo, mamia ya watu katikati mwa Tel Aviv, wameandamana hadi kituo cha kijeshi cha IDF mjini humo, wakiitaka serikali kuhakikisha inafikia makubaliano ili mateka waliosalia waachiliwe.
.
Miili ya watu hao watatu waliotambulika kwa majina ya Alon Shamriz, Yotam Haim na Samer Talalka, tayari imerudishwa katika ardhi ya Israel, ambapo ukaguzi ulithibitisha utambulisho wao. #via #BBC