Back to top

JAFO:TANZANIA YAFANYA VIZURI MWONGOZO HEWA UKAA

12 November 2022
Share

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dk. Selemani Jafo, amesema katika Mkutano 27 wa nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP27), Tanzania imekuwa ni nchi kinara katika uandaaji wa Mwongozo wa Biashara ya Hewa ya Ukaa.

Amesema hayo Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati wa Mkutano wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Bi. Zuhura Yunus, na waandishi wa habari kuhusu ziara ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, nchini China na Misri hivi karibuni.

Dkt. Jafo alisema hapo mwanzo hatukuwa na kanuni wala mwongozo wa biashara hii, na hivi sasa kukamilika kwake kutasaidia Tanzania kuweza kupata rasilimali fedha, za kupambana na mabadiliko ya tabianchi.