
Bi.Abigail Jo Shry, mkazi Houston katika Jimbo la Texas nchini Marekani ameshtakiwa kwa kutishia kumuua Jaji anayesimamia kesi ya jinai inayomkabili Rais wa zamani wa nchi hiyo Bw.Donald Trump, ambapo imedaiwa kuwa alipiga simu katika Mahakama ya Washington DC na kutumia lugha ya kibaguzi katika ujumbe wake kwa Jaji Tanya Chutkan.
.
Hata hivyo Bi.Shry amekiri kupiga simu hiyo baada ya wapelelezi kufuatilia namba yake, ambapo wamebainisha kuwa mwanamke huyo alimwambia Jaji huyo kuwa "Tunakutazama, tunataka kukuua".
.
Kulingana na jalada la Mahakama, waendesha mashataka wamesema, Bi.Shry pia alimwabia Jaji huyo kuwa "Ikiwa Trump hatachaguliwa 2024, tunakuja kukuua" huku pia akiwatishia Wanachama wa Democratic wote waliopo Washington DC na jumuiya ya LGBTQ.
