Back to top

Mwapachu aeleza chanzo kifo cha Mark Bomani.

11 September 2020
Share


Jaji Mstaafu Mark Bomani ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa kwanza wa Tanzania, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Aligaesha, amethibitisha na kusema kuwa Jaji Mstaafu Mzee Bomani alilazwa hospitalini hapo kwa siku 24

Marehemu Bomani alizaliwa 22 Oktoba 1943, Wete, Pemba na alikuwa ni mwanasheria mkuu kuanzia mwaka 1965 hadi 1976 wakati wa Utawala wa Rais wa Kwanza wa Tanzania, Julius Kambarage Nyerere.

Marehemu Bomani alifuatiwa na Joseph Warioba, hata hivyo amefariki akiwa ni jaji mstaafu ambaye ana kampuni binafsi ya sheria.