Back to top

JAMII YAHIMIZWA KUPAZA SAUTI VITENDO VYA UKATILI.

16 December 2022
Share

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu ,ameitaka jamii wadau kupaza sauti dhidi ya vitendo vya ukatili ambavyo vimekuwa vikiendelea katika maeneo mbalimbali nchini.

Amesema licha ya mafanikio yaliyopo kufuatia juhudi zinazofanywa kukabiliana na vitendo hivyo,  lakini bado ukatili umeendelea kufanywa, hivyo ipo haja ya kuwa na afua mbalimbali za kuwatetea manusura wa vitendo hivyo.

Dkt. Jingu ameyasema hayo Jijini Dodoma, wakati akifungua kikao cha Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu  Wakuu, kuhusu  mafunzo ya Usawa wa Kijinsia na Tathimini ya Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).