Back to top

Japan kutoa dola Bil. 30 kusaidia nchi za Afrika

28 August 2022
Share

Waziri Mkuu wa Japan, Fumio Kishida amesema nchi hiyo itatoa dola za Marekani Bil.30 ili kuziwezesha nchi za Afrika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na kuimarisha utunzaji wa mazingira.
.
Kishida, ameyasema hayo wakati akitoa hotuba kwenye Mkutano wa Nane wa Kimataifa wa Wakuu wa Nchi na Serikali unaohusu Maendeleo ya Japan na Afrika (TICAD8) unaofanyika katika ukumbi wa Palais des Congres, jijini Tunis nchini Tunisia.