Back to top

Jela kwa kuoa mke wa pili bila ruhusa ya mke wa kwanza.

22 June 2022
Share


Mahakama ya Pakistan imemuhukumu mwanaume aliyefahamika kwa jina la Saqib, kifungo cha miezi sita kwa kuoa mke wa pili bila ruhusa ya mke wa kwanza.

Mke wa mwanaume huyo Bi Ayesha Bibi, alishinda kesi hiyo, alipodai kuwa kitendo cha mume wake kuoa mke wa pili bila ruhusa yake kilikuwa ani ukiukaji wa sheria ya familia nchini Pakistan.