
Mahakama ya Wilaya ya Kigoma Mkoa wa Kigoma, imemuhukumu Baraka Michael (25) mkazi wa Rutale wilayani Kigoma kwenda jela miaka 30 baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka Bibi wa miaka 66.
Akitoa hukumu hiyo hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Kigoma Mheshimiwa Eva Mushi, amesema kuwa Mahakama imejiridhisha pasipo na shaka ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka na hatimaye kumtia hatiani mshitakiwa kwa kosa hilo.
Mshitakiwa huyo amehukumiwa kifungo hicho ili iwe fundisho kwa watu wanao jihusisha na vitendo vya ukiukaji wa sheria, maadili na ukatili dhidi ya wanawake.
