Back to top

JELA MIAKA 7 KWA KOSA LA WIZI WA MIFUGO

01 November 2023
Share

Mahakama ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma, imemhukumu kifungo cha Miaka 7 jela, Adam Said Mandanda (28) mkazi wa Kijiji cha Mchangani, Wilaya ya Tunduru baada ya kupatikana na hatia kwa kosa la wizi wa mifugo.

Hukumu hiyo ya kesi ya Jinai Na 127 ya mwaka 2023, imesomwa na Hakimu mkazi wa Mahakama hiyo Mhe. S.J Mwampashe, na kusema Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pasipo shaka yeyote.

Mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo 12 Oktoba, 2023 na kufikishwa mahakamani 25 Oktoba, 2023, sasa hukumu imetoka na kupatikana na hatia ya kosa hilo.