Back to top

JERRY SILAA AAHIDI KUPELEKA KAMATI KUTATUA MGOGORO, KIJIJI CHA MSANDA

19 November 2023
Share

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa, amewaahidi wananchi wa Kijiji cha Msanda Muungano kilichopo wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa, kuleta Kamati maalumu ya kushughulikia migogoro ya ardhi ya eneo hilo, ambayo itajumuisha wataalamu kutoka Makao Makuu Dodoma, Mkoa wa Rukwa, Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na wawakilishi wa wananchi.
.
Waziri Silaa amebainisha hayo baada ya Wakazi wa Kijiji cha Msanda mkoani humo, kuusimamisha msafara wa wake ili awasikilize na kutatua mgogoro wa ardhi wa muda mrefu.
.
Msafara huo wa Waziri Silaa uliosimamishwa na wananchi hao ulikuwa unaelekea Kijiji cha Sikaungu uliokuwa unaongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere , kuelekea kwenye mgogoro wa ardhi wa muda mrefu kati ya wananchi na Shirika la Efatha Ministry.
.
Mgogoro huo umekuwa ni chanzo cha uvunjifu wa amani na kupelekea mauaji ya kila mara jambo ambalo limelazimu wakazi hao kuomba Mhe. Silaa kuutatua mgogoro huo kwa haraka ili usiendelee kuleta madhala.