Jeshi la Ethiopia lamuua waziri wa zamani wa mambo ya nje.

Jeshi la Ethiopia limetangaza kuwa limemuua waziri wa zamani wa mambo ya nje Seyoum Mesfin, mmoja wa wanachama waanzilishi wa chama Tigray People’s Liberation Front (TPLF).

Bw.Seyum alihudumu kama waziri wa mambo ya nje wa toka mwaka 1991 hadi 2010, aliuawa pamoja na wanachama wengine wa ngazi ya juu TPLF kaskazini mwa jimbo la Tigray.