Back to top

JESHI LA GABON LAFUTA MATOKEO UCHAGUZI MKUU

30 August 2023
Share

Maafisa wa Jeshi la Gabon, wametangaza kufuta matokeo ya uchaguzi uliofanyika Jumamosi, ambao ulimtangaza Ali Bongo kama mshindi, katika nafasi ya Rais katika nchi hiyo.
.
Maafisa hao wametoa taarifa hiyo kupitia Kituo cha Runinga cha Taifa hilo, ambapo walibainisha kuwa Taasisi zote za serikali pia zimevunjwa, huku wakidai kuwa wameamua kulinda amani kwa kukomesha utawala uliopo.
.
Kupinduliwa Bw.Bongo kutakomesha utawala wa familia yake iliyodumu kwa miaka 53 madarakani nchini Gabon.