Back to top

JESHI LA POLISI: ASKARI WETU HAWAJACHEPUSHA FEDHA

29 May 2024
Share

Jeshi la Polisi nchini limekanusha taarifa za Askari wake kudaiwa kuchepusha fedha za Serikali, zilizotakiwa kuingia kwenye mfuko mkuu wa serikali kwa kuingilia mfumo wa malipo ya fedha za serikali POS (Point of Sale).
.
Kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa na Jeshi hilo, limefafanua kuwa, katika ukaguzi uliofanyika hivi karibuni lilibaini baadhi ya Askari wake walitumia mashine za kupima mwendokasi (Speed Radar) kinyume na maelekezo ya Jeshi hilo, na baada ya kubainika, walichukuliwa hatua za kinidhamu kwa kushtakiwa ambapo 8 walishafukuzwa kazi na kufutwa Jeshini na wengine kesi zao zipo katika hatua za mwisho. 
.
Limesema mashine zilizotumiwa kinyume cha utaratibu kwa utashi na kwa manufaa binafsi ya askari hao, ni za kupima mwendokasi na si zile zinazotumika kwa ajili ya malipo serikali (POS) ,kwani kuingilia mfumo huo si rahisi kama inavyoelezwa.
.
Aidha Jeshi hilo limewasisitiza Waandishi wa Habari wanapoambiwa wasubiri ufuatiliaji unafanyika na taarifa sahihi itatolewa wawe na uelewa na subira kwani wasipofanya hivyo ipo hatari ya kutoa taarifa zenye kuleta taharuki kwa umma bila sababu yeyote ile.