Back to top

Jeshi la Polisi lateketeza ekari 4 za bangi

22 May 2022
Share

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limeteketeza ekari nne na nusu za bangi katika eneo la Kisimiri juu, katika Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha ambapo Mkuu wa Operesheni za Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Gaudianus Kamugisha, amebainisha kuwa wameteketeza bangi yote iliyokuwa shambani na nyumbani ambayo ni kiasi cha gunia 10 pamoja na debe moja la mbegu ya bangi kwa kushirikiana na viongozi wa serikali ya vijiji.