Back to top

JESHI LA UHAMIAJI LIBORESHE HUDUMA ZAKE VIWANJA VYA NDEGE

30 November 2022
Share

Naibu Waziri wa Mmabo ya Ndani ya Nchi Mhe.Jummanne Sagini, amelitaka Jeshi la Uhamiaji nchini liboreshe huduma zake katika viwanja vya ndege, ili kupunguza malalamiko ya wageni kusimama kwenye foleni kwa muda mrefu kusubiri huduma.

Ametoa agizo hilo mjini Moshi alipozungumza na watendaji wa Jeshi la Uhamiaiji wa mikoa ya bara na visiwani nchini, waliokutana kujadili masuala ya utendaji ndani ya jeshi hilo.

Amewataka Maofisa wa Uhamaiji wawe na lugha nzuri kwa wageni wanaoingia na kutoka katika nchini, ili kuitangaza Tanzania vizuri kimataifa kupitia watalii wanaoingia na kutoka nchini.

Amelitaka jeshi hilo liwachukulie hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwaachisha kazi  watumishi watakaoshindwa kutimiza majukumu yao na kujihusisha vitendo vilivyo kinyume na maadili ya jeshi.