Back to top

Je,ulishawahi kuuchukia muonekano wa mwili wako?

14 May 2019
Share

Tafiti inaonyesha kuwa wasiwasi juu ya muonekano wa mwili umefanya idadi ya watu wenye huzuni kuongezeka na hata wengine kutaka kujiua.

Tamaa ya kuwa na Muonekano mzuri wa mwili kutokana na mtazamo wa kijamiii vyombo vya habari (matangazo ,watangazaji ),mitandao ya kijamiii yanatajwa kuongeza idadi ya watu wenye huzuni na wengine kufikiria hata kujiua huko nchini Uingereza.

Ambapo katika utafiti uliofanywa na Taasisi ya afya ya akili nchini Uingereza ‘The Mental Health Foundation’ amebaini kati ya watu wazima 4500 wamebaini robo ya watu hao hawajaridhika na muonekano wa mwili wao ,na mtu mmoja kati ya watu nane wamepata mawazo ya kujiua.

The Mental Health Foundation wamesema hali hii inaweza kumuathiri mtu wa rika lolote lile na   iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa madhara yanaweza kuwa makubwa zaidi.

zile taasisi ambazo zimekuwa zikitoa msaada kwa waathirika ambao wamekuwa wakiumizwa na hali hiyo ambapo wametoa rai kwa mitandao ya kijamii na hata matangazo mbalimbali yanayotengenezwa kuwa makini na namna wanavyotafsiri muonekano wa mwili mfano kutumia watu wa aina fulani labda mwembamba, mrefu, mweupe kutangaza aina fulani ya bidhaa kwani hili linaendelea kuleta mtazamo hasi katika jamii.