Back to top

JITUBOVU: NILIJUA MMEKUJA KUTUKAMATA KUMBE ELIMU

09 February 2024
Share

Kijana aliyejitambulisha kwa jina la Jitubovu, Mkazi wa Mtaa wa Makongoro uliopo Kata ya Sabasaba, Manispaa ya Morogoro amempongeza Polisi wa Kata hiyo, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Abubakary Jindu, kwa kuwapa elimu badala ya kuwakamata kama ilivyozoeleka, kuwa Polisi wanapofika kwenye maeneo ambayo vijana hao hukaa na kupanga uhalifu. 
.
Kijana huyo ameyasema hayo baada ya yeye na wenzake wachache waliobaki baada ya wengine kukimbia, kupewa elimu na Polisi Kata huyo. 
.
"Nilipoona Askari kwa mbali unakuja nikakimbia, lakini nilirudi baada ya kuona unapeana mikono na washkaji waliobaki, kumbe ni elimu mi nilijua ni kukamatana kama ilivyozoeleka mkija maeneo yetu" Alisema Jitubovu.
.
Aidha kwa upande wake Polisi wa Kata ya Sabasaba, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Abubakary Jindu amesema, walifika kwenye maeneo hayo ili kuwapa elimu vijana hao, ambayo itawasaidia kubadilika na kuacha vitendo vya uhalifu.
.
Miongoni mwa elimu waliyopewa vijana hao ni pamoja na madhara ya kutumia mihadarati, pombe kali ambazo hazijathibitishwa pamoja na miradi ya Polisi Jamii ikiwemo, Utii wa sheria bila shuruti na mada za ukatili.