Back to top

JKCI WAPEWA MSAADA WA VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA BIL. 1

11 July 2023
Share

Shirika la Madaktari Afrika, lenye makao yake nchini Marekani limetoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi bilioni moja, katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), ambavyo vitatumika katika kambi maalumu ya siku tano ya matibabu ya mfumo wa umeme wa moyo kwa watu wasiokua na uwezo, ambapo pia licha ya msaada huo madaktari hao watabadilishana uzoefu na wataalam wa afya wa JKCI.

Akizungumza na madaktari wanaotoa matibabu katika kambi hiyo, alipowatembelea kwenye Taasisi hiyo iliyopo mkoani Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Afya, Mhe.Dkt. Godwin Mollel aliwashukuru kwa msaada huo na kusema kuwa magonjwa ya mfumo wa umeme wa moyo ni sehemu ngumu kwenye masuala ya tiba ya moyo, huku akiwapongeza kwa kuwa mstari wa mbele kushirikiana na wataalam wa JKCI kuokoa maisha ya watanzania.