Back to top

JKT yajizatiti kutumia teknolojia bora na za kisasa katika uzalishaji.

26 February 2021
Share

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Charles Mbuge amesema jeshi hilo limejizatiti katika kuhakikisha wanatumia teknolojia bora na za kisasa katika uzalishaji wa mazao hali itakayowezesha jeshi kujitosheleza kwa chakula katika makambi pamoja na kulisha maeneo mengine.

Meja Jenerali Charles Mbuge ameyasema hayo katika Makao Makuu ya JKT wilayani Chamwino wakati jeshi hilo likiingia makubaliano ya mashirikiano na Wizara ya Kilimo katika kukuza sekta ya kilimo nchini.

Awali Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya amesema dhamira ya serikali ni kuhakikisha sekta ya kilimo inaendelea kukua hapa nchini kwa kutumia teknolojia bora na za kisasa.

Katika taarifa ilisomwa na Kanali Hassan Mabena ambaye ni Kaimu Mkuu wa Utawala JKT na pia Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ilibainisha baadhi ya vikwazo katika eneo la kilimo.