Back to top

JOSHUA ALIUAWA NA HAMAS BAADA YA KUTEKWA

14 December 2023
Share

Serikali ya Israel imeijulisha Tanzania kuwa Joshua Mollel, kijana wa Kitanzania aliyekuwa anasoma nchini humo aliuawa mara tu baada ya kutekwa na kundi la Hamas mnamo Oktoba 7, 2023.
.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe.January Makamba, amebainisha kuwa ameongea na Mzee Mollel, baba mzazi wa Joshua, kuhusu ujumbe huo, na kwamba wanafanya mpango wa awali wa kuwapeleka Mzee Mollel na mwanafamilia mwingine pamoja na Afisa wa Serikali, nchini Israel, kuungana na Balozi wa Tanzania nchini humo na maafisa waliopo huko, ili wakutane na kuzungumza na mamlaka za nchi hiyo ili kupata taarifa za ziada.