
Wakati hali ya Joto ikiwa kali katika maeneo mbalimbali nchini, Mamlaka ya hali ya hewa nchini imesema hali hiyo ya joto inatarajia kupungua pale mvua za masika zitakapoanza ambapo mamlaka hiyo itatoa utabiri wa mvua za masika siku chache zijazo.
Hayo yamebainishwa na Bi.Rozi Senyagwa, ambaye ni Mtaalam na Mchambuzi wa Hali ya Hewa Tanzania (TMA), wakati akizungumza na ITV Digital, ambapo amesema hali ya Joto kali ni kwamba kuna kuwa na hali ya unyevuunyevu wa kutosha angani, hivyo unyevuunyevu huo unahifadhi mionzi ya jua kwa kiwango kikubwa katika anga na hivyo kusababisha hali ya fukuto hata nyakati za usiku.
Bi.Rozi amesema kutokana na hali hiyo ya joto kali, wataalam wa afya wanashauri watu kunywa maji kwa wingi ili kupunguza hali ya joto, maana joto linapokuwa kali jasho linatoka kwa wingi.
