Back to top

JPM awanyooshea kidole wajumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM.

12 December 2019
Share

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Rais Dkt.John Magufuli amesema ndege ya Tanznaia iliyokuwa imeshikiliwa huko CANADA imeachiliwa.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa semina ya wajumbe wa Halamshauri Kuu ya Taifa ya chama hicho jijini Mwanza amesema ndege hiyo itapokelewa jijini Mwanza tarehe itakayopangwa.

Rais Magufuli amewataka wajumbe hao wa Halamshauri Kuu ya Taifa ya chama hicho waache kufanya kazi kwa mazoea, ili kuepuka kupoteza uhalalii wa kuongoza taifa.

Amewahimiza wapange mipango inayoakisi kujenga taifa linalojitegemea ambalo nguzo kuu za uchumii wake ni sekta ya viwanda, kutokanana utajiri mkubwa wa rasilimali zilizopo nchini.

Ametoa mfano wa aibu ya kuagiza viatu, maziwa, samaki na nguo kutoka nje ya nchi wakati uwezo wa kuzalisha hapa nchini ni mkubwa, amewataka waweke mipango itakayowezesha watanzania kutumia fursa hizo kukuza uchumi ili kujenga taifa linalojitegemea.

Katika hatua nyingne Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania, Isack Kamwelwe amesema mapokezi ya ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400 iliyokuwa imekamatwa nchini Canada yatafanyika Disemba 14, 2019 jijini Mwanza.