Back to top

JPM kuzindua shamba la miti ya kupandwa Chato.

26 January 2021
Share

Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mhe. Dk. John Pombe Magufuli kesho jumatano anatarajiwa kuzindua shamba la miti ya kupandwa la serikali wilayani Chato mkoani Geita ambalo ni la pili kwa ukubwa baada ya shamba la miti la serikali la Sao Hill lililoko mufindi mkoani Iringa.
.
Akiongea na waandishi wa habari wilayani Chato mkoani Geita mkuu wa mkoa wa Geita mhandisi Robert Gabriel amesema shamba hilo la miti la Chato lenye ukubwa wa zaidi ya hekta elfu sitini na tisa lililoanzishwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 ni miongoni mwa mashamba 23 ya serikali ya miti ya kupandwa yanayosimamiwa na kuendelezwa na wakala wa huduma za misitu nchini TFS.


Aidha  mkuu wa mkoa mhandisi Robert Gabriel amesema shamba la miti chato linalotarajiwa kuzinduliwa na Rais Dk John Pombe Magufuli limeanzishwa kutoka sehemu ya msitu mkubwa wa hifadhi wa Biharamulo Kahama uliohifadhiwa tangu mwaka 1954 ambao uliharibiwa kutokana na ongezeko la shughuli za binadamu ikiwemo kilimo, makazi na ufugaji.
.
Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Geita, pamoja na kuzindua shamba hilo la miti la Chato, Rais Magufuli anatarajiwa kuzindua miradi mingine ya maendeleo mkoani Geita ikiwemo kituo cha afya cha Masumbwe  kilichoko wilaya ya Mbogwe.